Baada ya Nay wa Mitego Kuchepuka na Msichana wa Kihabeshi… Lulu Diva Aliyekuwa Mpenzi Ahamia Kwa Belle 9


SIYO siri tena! Baada ya mkali wa Muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuchepuka kwa msichana wa Kihabeshi mwenye asili ya Ethiopia, aliyekuwa mpenzi wake Lulu Abass ‘Lulu Diva’ naye ameamua kugeukia kwa staa wa muziki, Abedinego Damian ‘Belle 9’.

Akizungumza na Over Ze Weekend Lulu ambaye ni muuza nyago kwenye video za Kibongo alidai kuwa, Nay hajatulia na badala yake anahitaji kuwa na mtu asiye na skendo za kutembea na wanawake ovyo na Belle 9 ndiye tulizo lake.

“Ni ukweli Nay nilikuwa naye kwenye uhusiano nikifahamu alishawahi kuwa na msururu wa wanawake lakini siyo siri yamenishinda na sasa nahitaji kujiweka kando. Sasa hivi feelings zangu zote zipo kwa Belle na analijua hilo,” alisema Lulu

Baada ya Nay wa Mitego Kuchepuka na Msichana wa Kihabeshi… Lulu Diva Aliyekuwa Mpenzi Ahamia Kwa Belle 9 Baada ya Nay wa Mitego Kuchepuka na Msichana wa Kihabeshi… Lulu Diva Aliyekuwa Mpenzi Ahamia Kwa Belle 9 Reviewed by on 11:18:00 PM Rating: 5