Msanii wa filamu Elizabeth
Michael ‘Lulu’ na Feza Kessy wamejitosa kwenye bifu la Shilole na Vanessa Mdee
ambalo linaendelea katika mitandao ya kijamii.
Chanzo cha bifu ya Shilole na Vanessa
hakijatambulika, lakini wawili hao toka jana wamekuwa wakirushiana maneno
makali na vitisho katika mitandao ya kijamii hali ambayo imewafanya baadhi ya
wasanii kuingilia kati sakata hilo la aina yake.
Muigizaji mahiri Elizabeth Michael
‘Lulu’ alikuwa moja kati ya msanii wa kwanza kutupia neno kwenye ugomvi huo kwa
namna ya kushangazwa na jinsi watu wanavyosifia uzuri wao kupitia mitandao ya
kijamii.
“Hebu nikazane kusoma nianze ligi za
kikubwa na dada zangu wenye madegree na ma masters kama ‘Esilovey’ hizi ligi
nyingine zinasikitisha,” aliandika Lulu kupitia Twetter huku akiongeza post
nyingine kwa kuandika “Watu wanashindania uzuri, makalio, followers, nguo,
outings, umaarufu, umaarufu wenyewe kama network ya mtandao unaokuwaga mpya,
full kukatakata,”
Pia msanii wa muziki na mtangazaji wa
Choice Fm, Feza Kezzy baada ya kuona stori inakuwa kubwa katika mitandao ya
kijamii, aliandika ya moyoni kuhusu jinsi watu wanavyo shabikia mambo yasiyo na
maana na kuacha kushabikia mambo ya msingi.
“Yaani watu wa ajabu sana, inabidi
mbadilike. Watu wakifanya mazuri or kazi nzuri hamsemi, hamsupport, lakini
umbea comments karibu laki moja dah. It’s very sad, bongo we need to change and
support our talents Not tear them apart, Ntawacheka sana mkigundua labda hata
ma star hawa hawana beef lol,” aliandika Feza kupitia instagram.
Feza na Lulu Wajitosa Kwenye Bifu ya Vanessa na Shilole
Reviewed by
on
11:04:00 PM
Rating: