Lema ambaye ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya nchi ameyasema hayo katika mahojiano maalum na EATV kuhusu maamuzi ya Rais kumng'oa Waziri Kitwanga katika wadhifa wake ambapo Lema amebainisha wazi kwamba Rais alipaswa kutengua uteuzi wa waziri huyo baada ya kuandamwa na kashfa ya ufisadi kwa kampuni ambayo ana ubia nayo ambayo ilipewa kazi ya kufanya manunuzi na kuweka mashine za kuhifadhi alama za vidole katika vituo vya polisi nchini.
''Bunge lilipuuzia maoni ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu suala la Waziri Kitwanga kuhusika katika kampuni iliyopewa kazi ya kuweka mashine katika vituo vya polisi, kama Rais alikuwa na nia njema angemsimamisha mapema kupisha uchunguzi, hii ya kuja kumsimamisha kwa maadili ya unywaji pombe ni issue ndogo ukilingnisha kashfa ya lugumi''-Amesema Lema.
Aidha Mbunge huyo ameeleza kuwa wakati wa Bunge la katiba pombe ilikuwa inauzwa bungeni hivyo kitwanga kusimamishwa kachukuliwa kama sample tuu kwakuwa wabunge na mawaziri wanaokunywa pombe wakati wa kazi ni wengi zaidi.
Rais Magufuli Alichelewa Kumng'oa Kitwanga -Lema
Reviewed by
on
6:37:00 AM
Rating: