Niliishia pale niliposema utakuta mwanaume anakuhesabia wanawake aliyokwishalala nao; Ester tayari, Jamila tayari, Jane pia, Suzana yeye juzijuzi tu. Halima zamani, Hawa tayari, sasa hivi namfukuzia Maimuna. Nikasema mwanaume wa hivi, anajua kutamani lakini si kupenda.
KASI YA KUFUKUZIA NI KUBWA KULIKO
Sifa ya tatu katika mada yangu ni kasi. Mwanaume mwenye sifa hii, kasi yake ya kumfukuzia mwanamke inatofautiana na kasi ya baada ya kumpata na kufanya naye tendo la ndoa.
Utakuta mwanaume anapofukuzia, atampigia simu mwanamke hata mara sita kwa siku. Meseji kila wakati, darling nyingi. Uko wapi usiseme. Wakati mwingine anataka kila siku jioni wakae wote. Na mwanaume wa hivi yu tayari kutumia gharama yoyote lakini si ya kudumu, ilimradi ampate mwanamke anayemtamani.
Lakini akishampata akalala naye hata mara moja tu, kasi inapungua. Walikuwa wanakaa wote kila jioni, sasa udhuru mwingi. Simu anaweza akapiga mara moja tu, akiulizwa anajibu; ‘simu yangu leo mchana kutwa haikuwa na salio. Vipi, mzima lakini wewe?’
Ila sasa, mwanaume anayetamani hana muda wa kumfukuzia mwanamke kwa muda mrefu, hukata tamaa mapema sana. Yaani hana muda wa kila siku anaenda naye sambamba. Kwa sababu hapendi, anatamani.
WANA IDADI KUBWA YA WANAWAKE
Kutamani ni kuona na kile unachokiona unakipeleka kwenye ubongo. Mwanaume wa hivi akishamwona mwanamke mbele yake, anampeleka hadi kitandani. Atakavyokuwa akimpa mahaba, akimfanyia hili na lile. Hapo ndipo kutamani huanzia.
KWAO TABIA NJEMA SIYO ISHU
Sifa nyingine ya mwanaume anayetamani ni kutoangalia sifa ya tabia njema kwa mwanamke. Kama tamaa yake imelala kwenye wowowo kubwa basi ataganda hapo. Kama imelala kwa wanawake mijimama, basi ataganda hapo. Kwa sababu ndipo penye kipaumbele chake.
WASICHOKIJUA WANAWAKE
Hata hivyo, wanawake wengi wanajikuta wakiangukia kwenye uhusiano na wanaume wanaotamani kwa sababu hawajui kuwatofautisha.
Wanawake wengi wanaolia kwa sababu ya kukutana na wanaume waliowatamani ni wale waliojirahisi kwa muda mfupi sana. mwanaume kama anakupenda kwa dhati, hawezi kukata tamaa katika kukufukuzia. Iwe mwezi, miezi na hata mwaka! Wapo wanaume wa hivi.
Kwa wewe mwanamke, ukikutana na mwanaume mwenye mambo hayo matano, jua ana dalili za kukutamani na si kukupenda, shituka.
Sehemu ya Pili: Sifa tano za mwanaume anayekutamani
Reviewed by
on
10:46:00 PM
Rating: