CONFIRMED: Man United imemsajili Eric Bailly leo June 8 2016


Klabu ya Manchester United ya Uingereza leo June 8 2016 imefanikiwa kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Ivory Coast aliyekuwa anaichezea klabu ya Villarreal  ya Hispania Eric Bertrand Bailly.
Man United imefanikiwa kumsajili Eric Bertrand Bailly kwa mkataba wa miaka minne, mkataba ambao una kipengele cha kumuongezea miaka miwili zaidi, Eric Bailly alijiunga na Villarreal January 29 2015 na ameichezea jumla ya mechi 47 na mechi 15 kaichezea timu yake ya taifa ya Ivory Coast.
Bailly mwenye umri wa miaka 22 alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa Ivory Coast waliofanikiwa kutwaa Kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2015 na alicheza jumla ya mechi zote sita za mashindano hayo.
ALL GOALS: TAIFA STARS VS MISRI JUNE 4 2016, FULL TIME 0-2

CONFIRMED: Man United imemsajili Eric Bailly leo June 8 2016 CONFIRMED: Man United imemsajili Eric Bailly leo June 8 2016 Reviewed by on 7:49:00 AM Rating: 5