Mtoto wa Ajabu Mwenye Vichwa Viwili Azaliwa Geita



WANANCHI katika kijiji Kaseke kata ya Kasami wilayani na Mkoani Geita wamekubwa na taharuki na wasiwasi mkubwa mara baada ya  Geresi Saidi( 20) Kujifungua mtoto wa kiume mwenye vichwa viwili vinavyofanana sura.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jumapiri majira ya saa sita usiku katika katika kituo cha afya katoro alikwenda kujifungua muda mfupi baada ya kupata uchungu.

Channel Ten ilifika kijiji hapo na kushudia viumbe hao huku mamia yawananchi kutoka kila kona  wakifika na kushudia  tukio hilo na hapa mashuhuda wakaeleza ilivyokuwa.

Baba mzazi wa mtoto huo Stefano Lugisha amesema pamoja na mke wake kujifungua mtoto huyo lakini  ana imani kama ni mipango ya mungu kama amavyoeleza.

Diwani wa kata hiyo Anderea Karamura pamoja na mwenyekiti wa kijiji Zakaria Rukas wamewataka wananchi wao kutoliusisha tukio hilo na imani za kishilina swara hilo.

Akiongea kwa njia ya simu mganga kitua hicho aliyempokea mama huyona kumzalisha  Peter Janga amedhibitisha kutokea kwa na kwamba uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini nini tatizo kwa mama huyo ambaye hiyo ilikuwa ni nzao ya kwanza na kuongeza kuwa kiumbe hicho kilipoteza maisha baada ya muda mfupi.
Mtoto wa Ajabu Mwenye Vichwa Viwili Azaliwa Geita Mtoto wa Ajabu Mwenye Vichwa Viwili Azaliwa Geita Reviewed by on 5:02:00 AM Rating: 5