Muigizaji wa filamu nchini Tanzania katika tasnia ya Bongo Movie, Rose Ndauka, amejikuta akijing’ata ng’ata kuhusiana na ahadi aliyo iahidi kuwa ataanza kuwasimamia wanamuziki wa Bongo fleva.
Akizungumza na eNewz ya EATV, Rose Ndauka alisema kuwa mpango wake wakuwasimamaia wanamuziki wa Bongo fleva bado upo, Lakini alishindwa kujieleza kuhusiana na uwezo wake wa kusimamia wasani hao nakusema kwa sasa hana ujuzi wowote na anajifunza kwanza.
Pia alipoulizwa kuhusiana na wasanii wa filamu Tanzania kuonekana wanavaa nguo fupi zaidi, Rose Ndauka alifunguka kuwa hakuna tatizo kwa mtu kuvaa nguo fupi lakini kama mtu ana mguu mzuri nisawa akavaa.
Video: Rose Ndauka ajing’ata ng’ata kuhusu ahadi yake ya kusimamia wasanii huku...
Reviewed by
on
6:52:00 AM
Rating: