Uhusiano wa sasa wa msanii wa filamu na muziki Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na mwanaume wake umetibuliwa na Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm baada ya hivi karibuni kukutana naye maeneo ya Coco Beach jijini Dar kisha kupiga picha ya ‘ziro distance’.
Kutibuka penzi la Kabula na ‘mtu wake’ kumekuja kufuatia watu waliowaona msanii huyo na Pluijm wakipiga picha hizo kumfikishia ubuyu mpenzi wa Kabula (jina halikufahamika mara moja) aliyeonesha kumaindi na kumuanzishia kasheshe Kabula.
Licha ya wambeya kumtonya baby wa Kabula juu ya picha hizo, wapo waliozitupia mtandaoni wakionesha kuwa mwanadada huyo kajiweka kwa kocha huyo, jambo ambalo halina ukweli.
Akizungumza nasi mara baada ya picha hizo kutupiwa mtandaoni kisha kila mmoja kusema lake, Kabula alisema kuwa anawashangaa Wabongo kwa kuzusha mambo kwani hakuna lililoendelea wala lililo nyuma ya pazia zaidi ya kupiga picha tu.
“Yaani watu wamefanya hadi penzi langu limeyumba, baby wangu kamaindi na kuhisi labda nimejiweka kwa kocha wa timu yangu ya Yanga kutokana na meneno ya watu walioweka picha hizo mtandaoni na kuandika wanayojua.
“Niseme tu kwamba mimi ni shabiki damu wa Yanga, nimepiga hizo picha kutokana na ushabiki wangu lakini hakuna chochote,” alisema Kabula aliyewahi kuripotiwa kuwa kwenye uhusiano na mchezaji mmoja wa kigeni wa Timu ya Yanga.
Kabula na Pluijm walikutana kwenye Ufukwe wa Coco ambapo msanii huyo alikuwa ameongozana na wasanii wenzake, Baby Madaha, Isabela Mpanda na Mama Loraa kwenda kufanya shooting ya wimbo wao wa Marioo huku kocha huyo akiwa eneo hilo na timu yake kwa ajili ya mazoezi.
Penzi la Jini Kabula kutibuliwa Kocha wa Yanga SC
Reviewed by
on
11:38:00 PM
Rating: