MIRIAM Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka sababu iliyomfanya ashindwe
kufunga ndoa na mzazi mwenzake Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuzi’ ni wosia
kutoka kwa wazazi wake ambao walimwamru kutobadili dini yake ya
Kikristo.
“Nilishaapa siwezi kubadili dini kwa ajili ya Ndoa hata nilipozaa na
Mr. Chuzi kikwazo ilikuwa dini siwezi kupingana na wosia wa marehemu
Baba yangu,”anasema Kabula.
Kabula anasema kuwa anachofurahia ni yeye kufanya kazi na mzazi
mwenzake kwa heshima kwani kwa sasa anamchukulia kama bosi wake na si
mume wala mtu ambaye ana malengo nayo kwa ajili ya kuishi naye kama mke
na mume zaidi ya kufanya kazi tu.
Jini Kabula alikuwa na mahusiano na mtayarishaji na muongozaji wa
filamu na tamthilia Swahilihood Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuzi’ na
walifanikiwa kuzaa mtoto wa kike ajulikanaye kwa jina la Salma Kihangala
ambaye pia anafuata njia ya wazazi wake katika uigizaji.
Dini imesababisha Nisifunge Ndoa na Chuzi Zaidi ya Kuzaa Naye Tu- Jini Kabula
Reviewed by
on
11:23:00 AM
Rating: