Naanza kwa kuwasalimu kwa JINA LA YESU. Jina lililo Kuu kupita majina yote.
Wiki kadhaa zilizo pita, niliandika waraka wangu kwa watanzania na kuusambaza kupitia blogs na mitandao mbalimbali kuhusu athari za kujihusisha na masuala ya waganga wa jadi .
Katika waraka huo niliwatahadharisha watanzania kutojihusisha na WAGANGA WA TUNGULI kwa sababu WAGANGA WA TUNGULI ni WACHAWI NA MAWAKALA WA SHETANI walio vaa kofia ya utabibu.
Katika waraka huo niliwaelezea watanzania jinsi nilivyo shawishika kutafuta msaada wa maisha yangu kwa MGANGA WA TUNGULI aitwae MUNGU WA KABILI na kujikuta nikipata matatizo makubwa ambayo hata hivyo yalipelekea kunikutanisha na YESU ambae ameniokoa.
Katika waraka huo nili sahau kueleza mambo makuu mawili yafuatayo:
Kwanza nilisahau kuweka mawasiliano ya MUNGU WA KABILI ayatumiayo pindi anapokuwa nchini KENYA ili kuwa tahadharisha wakenya wasipige namba hiyo wala wasijaribu kutafuta msaada kwenye namba hiyo, kwa sababu mtu huyo ni WAKALA WA SHETANI alie jificha kwenye kivuli cha UGANGA...
Wengi walio jaribu kutafuta msaada kwa MUNGU WA KABILI wamejikuta wakiishia kuunganishwa na UTAWALA WA KUZIMU ambao umewapelekea kujikuta katika matatizo makubwa kama niliyo yapata mimi.
Nimeona vyema kuwatahadharisha wakenya, kwa sababu mungu wa kabili hufanya kazi zake Tanzania na Kenya. Anapokuwa Tanzania, namba yake huwa ni + 255 744 000 473 na anapokuwa Kenya , namba yake huwa ni + 254 704 71 61 59.
Hivyo basi Ndugu zangu Wakenya , hii ni tahadhari yangu kwenu. Nimeweka namba hizo hapo juu kama alama ya MPINGA KRISTO ambayo watu wote wenye hofu ya Mungu wanapaswa kuepukana nayo..
Nimeongozwa katika namna ya rohoni, kuanza kufanya kampeni ya nguvu dhidi ya roho ya kuhusudu masuala ya UGANGA, UCHAWI NA USHIRIKINA na nitajikita zaidi katika mapambano dhidi ya MGANGA WA JADI AITWAE MUNGU WA KABILI.
Ninaanza kwa kupambana na MUNGU WA KABILI kwa sababu, kwa miaka zaidi ya mitatu ambayo nimekuwa nikishirikiana na MUNGU WA KABILI, nimeweza kujua kuwa yeye ndio MKUU WA WAGANGA NA WACHAWI WOTE WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI , na watu wenye hekima wanasema katikati ya kundi la kondoo MPIGE RUNGU MCHUNGAJI, NA KONDOO WOTE WATATAWANYIKA.
Naamini nikimsambaratisha mungu wa kabili, basi itakuwa rahisi kwa waganga wengine kwa sababu wote ni kama wafuasi wake tu.
Katika kampeni yangu hii ya kiroho, nimeanzisha blogu iitwayo SHUHUDA ZA AJABU ambayo inapatikana :www.shuhudazaajabu.blogspot. com.
Nitakuwa nikitoa shuhuda za mambo mbalimbali ya kichawi niliyo fundishwa na MUNGU WA KABILI na jinsi unavyo weza kujiepusha nayo kwa kutumia Jina la Yesu.
Najua kazi hii itainua uadui mkubwa dhidi yangu, kwa sababu hakuna kitu wachawi wanakichukia kama siri zao kutolewa hadharani, lakini kwa Jina la Yesu, nitapambana vita hii na nitaishinda.
MUNGU WA KABILI na jeshi lake watajaribu kushindana na mimi lakini hawatashinda.( YEREMIA 1:19.)
Shuhuda nitakazo zitoa, zitakuwa na mafundisho mazuri yatakayo kupa faida , kama Mungu anavyo sema katika kitabu cha ISAYA 48 kwamba " MIMI NI MUNGU NIKUFUNDISHAE ILI UPATE FAIDA'.
Ushuhuda huu utakufanya umjue shetani vizuri kama wasemavyo watu wenye hekima " MJUE ADUI YAKO KAMA UNAVYO IJUA NAFSI YAKO"
JAMBO LA PILI na la msingi ambalo sikuweza kulielezea kwa kina katika waraka wangu wa kwanza ni namna ambavyo MUNGU WA KABILI alinifundisha uchawi na uganga...
Nianze kwa kurudisha kumbukumbu zenu nyuma. Kama mlifatilia vizuri waraka wangu mtakuwa mnakumbuka kuwa, kwa kutumia uchawi nilio pewa na MUNGU WA KABILI, nilifanikiwa kuteka na kudhulumu mali za mwanaume mume wa mtu aitwate " K".
Mali hizo zilikuwa ni pamoja na maduka mbalimbali ya biashara ambayo nilimkabidhi mdogo wangu ayasimamie.
Kutokana na usimamizi wa hovyo ulio fanywa na mdogo wangu, maduka hayo yakaanza kufilisika taratibu. Hali hii ilinifanye niende kuomba msaada wa MUNGU WA KABILI.
Mungu wa Kabili akaniambia kuwa mimi siwezi kufanikiwa kupitia biahsra yoyote hata iweje. Mungu wa Kabili akaniambia , Nina nyota ya Uganga " kwa hiyo ninatakiwa kuwa mganga.
Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana nae kwa sababu nilishamfanya kuwa kama muungu wa maisha yangu. Nilitii na kufuata kila alicho kisema.
Ikapangwa siku rasmi ya mimi kusimikwa uganga kisha baada ya kusimikwa uganga ndipo nianze kufanya kazi ya kuwaagua watu wenye shida, tabu na matatizo mbalimbali ya kimaisha.
Zoezi la kunisimika uganga rasmi lilikamilika ambapo nilikabidhiwa nyenzo za uganga pamoja na jina la kazi, baada ya hapo, mungu wa kabili akaniambia, nitaanza kufundishwa uganga, lakini akasema, kabla ya kuujua uganga ninatakiwa kuujua kwanza uchawi, kwa nadharia na vitendo. Hapo ndipo ninaposema siku zote kuwa MCHAWI NA MGANGA LAO MOJA.
mungu wa kabili aliniambia ' UCHAWI NI SAYANSI YA SIRI YENYE MRENGO WA UFISADI ( YANI MLENGO WA UHARIBIFUI ) Ilihali UGANGA NI SAYANSI YA SIRI YENYE UWEZO WA KUPAMBANA ATHARI ZA NGUVU YA SAYANSI YENYE MLENGO WA UFISADI.
mungu wa kabili akaniambia, ili niwe na uwezo wa kupambana na uchawi ni lazima kwanza niufahamu uchawi vizuri kwa nadharia na vitendo , kisha baada ya hapo nitafundishwa kuhusu mbinu za kupambana na uchawi ambao kwa mujibu wa mungu wa kabili, ndio huo uganga wenyewe..
Nilifundishwa vitu sana katika uchawi, kuanzia jinsi ya kuroga ukoo mzima, kufanya watoto wasikue, kutengeneza ukimwi wa kichawi, kuvunja ndoa, kutengeneza radi, nyoka, simba n.k, kusafiri na aina tatu za ungo wa kichawi, kutengeneza na kuzuia mvua, kuchukua misukule, kutengeneza magonjwa mbalimbali kwa watu, mimea na mifugo, kutengeneza chuma ulete, kutengeneza majini,kuingia mikataba na majini & mizimu, kuwafunga watu vifungo vya kichawi vya aina mbalimbali nakadhalika....
==>
MUNGU AKUBARIKI SANA..AMEN
Tahadhari Kwa Wakenya : Uchawi Ni Utumwa.
Reviewed by
on
10:46:00 PM
Rating: