Kilio cha Maisha Magumu: Je, Tulikuwa Tunategemea Vipato Haramu?


Kuna kilio cha maisha magumu kila kona. Utasikia wakina mama,wafanyakazi, vijana hata wazee wanadai kipindi hiki cha awamu ya tano pesa imekuwa ngumu sana!.

Ninajiuliza;
1:Serikali inatueleza Inazuia ufisadi, kubana matumizi yasio ya lazima, matokeo yake wananchi wanalia eti maisha yamekuwa magumu maana yake nini?

2:Makusanyo ya Kodi ya kuwahudumia wananchi yameongezeka sana lkn kilio kila kona, tatizo nini?

3:Je Maisha bora mtaani kipindi kilichopita yalikuwa matokeo ya wizi,ufisadi,matumizi mabaya ya pesa za umma na ukwepaji kodi?

4: Nasikia hotel zinakoswa wateja na taasisi nyingi zinazorota kutokana na kubana matumizi kwa serikali. Najiuliza hivi hawa jamaa walianzisha hizo taasisi/kumbi/hotel walikiwa na market strategy ya kutegemea wateja wawe serikali tu au?

5: je, unadhani nini kinakosekana ili kikiwepo Mafisadi waendelee kutumbuliwa,wakwepa kodi walipe, Gharama za maisha zishuke, Serikali iwe na pesa za kutosha, n.k na maisha ya wananchi yawe saaafi kwa matajiri na maskini kihalali? nini kinakosekana.

Najaribu kuwaza....
Kilio cha Maisha Magumu: Je, Tulikuwa Tunategemea Vipato Haramu? Kilio cha Maisha Magumu: Je, Tulikuwa Tunategemea Vipato Haramu? Reviewed by on 11:28:00 PM Rating: 5