Julai 16, 2016 simu feki zitazimwa, Bofya hapa kujua kama simu yako ni fake au original


Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Juni 16, 2016 inatarajia kuzima simu zote feki nchini. Hii ni kufuatiwa taarifa iliyotolewa na wataalamu wa mamlka hiyo kuwa simu hizo zina madhara makubwa sana kwa watumiaji wake kwa sababu zipo chini ya viwango vinavyotakiwa.

Kumekuwa na watu wengi wakijiuliza kama simu zao nao zitazimwa au la kwa sababu hawana uhakika kama nazo ni miongoni mwa simu feki au la. Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania imetoka utaratibu ambao kila mmoja anaweza kuangalia kama simu yake/zake ni feki au original.

Namna ya kuhakiki IMEI ya simu yako kujua kama ni feki au sio feki.

Piga *#06# kwenye simu yako ya mkononi. Namba itakayoonekana kwenye simu yako inaitwa IMEI na haifanani na ya simu nyingine yoyote. Kwa simu zenye kadi za simu mbili (laini mbili) simu yako itaonyesha IMEI mbili.

Kisha tembelea bofya link hii http://www.tcra.go.tz/index.php/imei-code-verification na namba iliyojitokeza baada ya kupika *#06# utatakiwa kuiingiza kwenye sanduku (box) lililowazi kisha bonyeza kitufe kilichoandikwa “verify my device”. Baada ya kubonyeza, kampuni iliyotengeneza simu yako, itaonekana hapo kutokana na namba itakayokuwa umeinginza na itakuonyesha kama simu yako ni feki au sio feki.

Kama simu yako ni feki, chukua tahadhari mapema kwani ni mwezi mmoja tu umesalia kabla simu hizo hazijazimwa. Mshirikishe mwingine.
Julai 16, 2016 simu feki zitazimwa, Bofya hapa kujua kama simu yako ni fake au original Julai 16, 2016 simu feki zitazimwa, Bofya hapa kujua kama simu yako ni fake au original Reviewed by on 2:23:00 AM Rating: 5