Msanii Dayna Nyange mwezi uliopita alihudhuria ndoa ya mshkaji wake
Roma ilifanyika mjini Tanga, lakini pia mwezi uliopita kuna picha yake
ilisambaa anaonekana ametupia shela la harusi yupo na mwanaume flani,
akiizungumzia picha hiyo alisema kuwa picha ile ilipigwa kwenye
maonyesho ya mavazi, je ana mtazamo gani kuhusu ishu za kufunga pingu za
maisha.
‘’Kiukweli kabisa kuna wakati natamani niwe kwenye mahusiano natamani
niwe naamka na mume wangu,naenda sehemu Fulani lakini najua nimemuacha
mume wangu,yaani niwe mwanamke ambaye nina mume wangu,lakini kwa
mazingira yetu ya sasa hivi yanatuwia vigumu sana kuamua au kuingia
kwenye mahusiano hayo kwa sababu kadhaa yawezekana vijana tumekuwa na
tamaa nyingi au watu wamekuwa waoga wa maisha wanajikuta wamekuwa waoga
kwenye mahusiano ya ndoa’’ Alisema Dyna.
‘’Kuna wanawake pia siku hizi wamekuwa wakijirahisisha sana uko na
mwanaume umekutana nae mwezi mmoja unataka akuoe, unawezakukuta mwanaume
anataka kukuoa lakini hujamridhia ilishawahi kunitokea kama mara tatu
najikuta nakuwa muoga kwasababu nyingi ambazo nimepitia katika maisha
yangu kabla kwahiyo nakuwa muoga kufanya maamuzi hayo ya kuingia kwenye
ndoa kwa kutamani tu, kuna vitu vichache unatakiwa uviangalie na
uvikubali kabla ya kuingia kwenye ndoa sasa unakuta havipatikani au
unakuta viko nusu mwisho wa siku tunakuwa kwenye mahusiano tu ya
kawaida’’ Alisema Dyna.
Msanii Dayna Atoboa Sababu za Kukataa Kuolewa Mara Kadhaa
Reviewed by
on
11:33:00 PM
Rating: