UHUSIANO wa wasanii wawili wa
filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Geofrey Kusila umeota mbawa baada
ya kumwagana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.
Chanzo kilicho karibu na wasanii hao kimepenyeza habari kuwa uhusiano wao umevunjika bila kufahamika chanzo.
“Nora
na Geofrey wameshaachana na kila mtu ana maisha yake hata kazi
hawafanyi tena pamoja, tangu walipoachana Nora anaandaa kipindi chake
kwenye runinga na hayupo tena na Geofrey,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Nora ili kuujua ukweli, akafunguka:
“Mimi
ninafanya kazi zangu mwenyewe na Geofrey kivyake kwa sababu tumeachana
na kampuni ambayo tulikuwa tumeianzisha nayo imekufa na baada ya hapo
kila mmoja akashika njia yake na kuangalia jinsi gani atakavyofanya
kazi hivyo hatupo pamoja tena.”
UHUSIANO WA WASANII NORA NA GEOFREY KUSILA WAVUNJIKA....
Reviewed by
on
11:36:00 PM
Rating: