Msanii TID amefunguka na kusema kuwa kuna watu ambao bado wananufaika na kazi za marehemu Albert Mangwea kwa kuuza kazi hizo bila hata mama wa msanii huyo au familia kuhusishwa, japo yeye mwenyewe anasema anaamini yapo makampuni ambayo huenda mama Ngwea labda atakuwa anapata chochote kitu kutokana na kazi za mtoto wake ambazo zinaendelea kuuzwa na kutumika kama kwenye mitandao mbali mbali ya simu.
TID ameonyesha wasiwasi mkubwa kuwa kuna kundi la watu ambao linanufaika na kazi za Ngwea na kusema kwamba wapo wasanii wapo hai lakini kazi zao bado zinaibiwa na wajanja hivyo anaamini huenda kazi za marehemu Ngwea zitakuwa zikiibiwa zaidi pasipo familia kunufaika na lolote.
"Najua unapo saini mikataba kuna watu ambao unaweza kuwaweka kama wanufaika wa kazi zako pindi unapokuwa umefariki kwa sasa naamini labda Mama yake na Ngwea ndiye mnufaika wa kazi za mwanaye japo sina uhakika kama ananufaika, unajua Tanzania hii ni hatari sana TID Mnyama nipo hai lakini kazi zangu zinaibiwa, atakuwa Ngwea, ehhh Mwana FA na AY wanaibiwa kazi zao na wajanja atakuwa mtu ambaye amefariki?" alihoji TID.
- EATV
TID alia kwakusema AY, Mwana FA wako hai wanaibiwa itakuwa Ngwea!
Reviewed by
on
8:07:00 AM
Rating: