TUHUMA za ubadhirifu wa Sh bilioni 1.4 za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma, zimefikishwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga, alisema Takukuru inakamilisha uchunguzi wa kina ili wahusika waliofanya ubadhirifu huo wachukuliwe hatua za kisheria.
Alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema upo ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliofanywa na wahusika waliopewa dhamana ya kusimamia matumizi yake.
Ngaga alisema, ofisi yake baada ya kuunda tume ndogo na kubaini hilo, uchunguzi wa awali unaonesha Sh milioni 513 zimefanyiwa ubadhirifu .
Alisema, aliona ni vyema achukue hatua ya kukabidhi tuhuma hizo kwa Takukuru wafanye uchunguzi wa kina kutambua ni nani aliyehusika na ubadhirifu huo.
Alisema, taarifa na majina ya wahusika waliofanya hivyo itatolewa baadaye Takukuru ikikamilisha kazi yake.
“Takukuru inaendelea na uchunguzi, ikikamilisha taarifa itatolewa. Katika maelezo yangu ya awali kwenye Baraza la Madiwani lililokaa juzi sikuhukumu mtu wala kusema amehusika, hivyo tusubiri tutajulishwa,”alisema.
Aliongeza kuwa, uchunguzi huo utakapokamilika, taarifa husika zitapelekwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu awasilishe kwa Waziri mwenye dhamana.
Awali, tuhuma za ubadhirifu huo, zilitolewa na Mkuu wa Wilaya kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa wilaya hiyo, Mei 11, mwaka huu.
Tuhuma za Ubadhirifu wa Sh bilioni 1.4 za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana Zatua TAKUKURU
Reviewed by
on
3:13:00 AM
Rating: