Bi Mwenda kuacha Uigizaji kwa sababu ya Uzee


MUIGIZAJI mkongwe kwenye Tasnia ya Filamu Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ amefunguka kuwa anaona uzee umeshamfikia hivyo muda si mrefu ataamua kupumzika kuigiza ili afanye kitu kingine kulingana na umri wake.

Akizungumza nasi, Bi Mwenda alisema amecheza filamu muda mrefu takriban miaka ishirini hivyo anaona wazi atashindwa kukimbizana kwenye kambi kwenda huku na huko kutokana na umri wake hivyo anajipanga kuangalia afanye nini.

“Kweli kabisa nikijiangalia uzee umeshagonga hodi na siwezi kuukimbia ila kwa sasa najipanga nipumzike kwani ni muda mrefu niko kwenye sanaa, nitaangalia nifanye nini ili kipato changu kiendelee,” alisema Bi Mwenda pasipo kuainisha atasimama baada ya muda gani.
Bi Mwenda kuacha Uigizaji kwa sababu ya Uzee Bi Mwenda kuacha Uigizaji kwa sababu ya Uzee Reviewed by on 12:26:00 AM Rating: 5