Staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford ‘Chausiku’ anayedaiwa kujitwalia mwanaume aitwaye Chid Mapenzi huku nyuma yake kukiwa na mazito kwamba, mwanaume huyo aliwahi kumilikiwa na mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’.
Kumekuwa na habari za chini kwa chini kuwa Shamsa anatoka na Chid Mapenzi ambaye ni mfanyabishara wa jijini Dar ambapo hivi karibuni, mwanamama huyo alitupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mwanaume huyo.
Katika picha hizo ambazo chanzo cha uhakika kinashikilia ‘nakala’ zake, Shamsa anaonekana akijiachia na Chid Mapenzi huku akiwa amemziba sura.
Ilidaiwa kwamba, bidada huyo alidhani watu hawatamtambua jamaa huyo lakini ‘watu wabaya kwa ubuyu’ ambao wanamjua vizuri Chid Mapenzi, hawakusita kuchukua hatua kwani ndani ya dakika sifuri walitupia jina lake na picha za tatuu yake kuonesha ushahidi kuwa ni yeye.
Baada ya kutajwa kwa jina hilo ndipo yakaibuka maneno mengi ikiwa ni pamoja na kejeli za kumsema Shamsa kuwa ‘amepotea’ kwa mwanaume huyo kwani alishakuwa na uhusiano wa kupika na kupakua na Wolper.
Kama kawaida, Mwandishi wa Ubuyu alifuatilia sakata hilo hatua kwa hatua ili kubaini ukweli kama Wolper aliwahi kutoka na Chid Mapenzi.
Katika ufukunyuzi wa hali ya juu, ilibainika kwamba, kuna ukweli ambao ulipatikana kupitia marafiki wa karibu wa Wolper.
Huku akiomba hifadhi ya jina, mmoja wa marafiki hao wa Wolper alimhakikishia mwanahabari wetu kuwa hakuna shaka kwamba Wolper alishakuwa mtu wa Chid Mapenzi lakini ni kitambo kidogo.
“Ni kweli hata yeye (Wolper) hawezi kubisha kwa sababu amekuwa na Chid japokuwa ni zamani kidogo.
“Wapo wanaosema walimwagana lakini wakarudiana kisha wakaachana tena ila mimi hilo la kumwagana na kurudiana kisha kumwagana tena sina uhakika nalo lakini ukweli ni kwamba walikuwa wakipendana mno hadi wakawa kero kwa baadhi yetu,” kilinyetisha chanzo hicho.
Kama Wolper na Chid walikuwa wapenzi enzi hizo, hilo halimzuii Shamsa kuwa na uhusiano na mfanyabiashara huyo. Kibaya ingekuwa ni kama Shamsa angeingilia penzi hilo likiwa hai kwani tujuavyo mwanamke kama hajaolewa anaweza kuolewa na mwanaume yeyote na pale Mungu alipokupangia huwezi kupangua.
Ila nawasihi wasanii kuchunguza wanaume kabla ya kuingia nao kwenye mapenzi ili kuepusha kuhesabiwa idadi ya wanaume kwani Shamsa hajui sababu za Wolper kuachana na bwana huyo na yeye inawezekana ameingia kwa lengo la kutafuta ndoa baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke, Dickson Matoke ‘Dick’ aliyezaa naye mtoto wa kiume, Terry.
Shamsa Ford Adaiwa Kuiba Bwana wa Walper
Reviewed by
on
11:45:00 PM
Rating: