Baada tu ya kutoka kurekodi collabo ya Coke Studio ZA na Cassper Nyovest, Diamond Platnumz aliingia location kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na staa wa Zimbabwe, Jah Prayzah.
Prayzah ambaye jina lake halisi ni Mukudzei Mukombe alilazimika kusafiri hadi Dar es Salaam kuja kukamilisha collabo yake na Diamond hivi karibuni.
Jah Prayzah ambaye hujulikana pia kwa jina la Musoja kutokana na kupenda kuvaa nguo za kijeshi, amemshirikisha Diamond kwenye wimbo wake uitwao Watora Mari.
Wimbo huo utapatikana kwenye album yake mpya na ya saba, iitwayo Mudhara Vachauya itakayozinduliwa August 12.
Diamond ameshare picha Instagram akiwa na staa huyo na kuandika: Wraping it up my Zimbabwean brother @jahprayzah Video #Kidogo before spending time with my Miss world!”
Akiongea na gazeti la The Zimbabwe Standard mwishoni mwa mwezi uliopita, Jah Prayzah alisema ameamua kumshirikisha Diamond kutokana na umaarufu wake barani Afrika.
“Ni nzuri kushirikiana na watu maarufu kama hao barani kwasababu watu wengi zaidi watakufahamu kupitia yeye na ni suala la kusaidiana ili kwenda mbali zaidi,” alisema.
Wimbo huo ulirekodiwa kwenye studio za Wasafi jijini Dar es Salaam na staa huyo hakusita kuelezea furaha yake kwenye Instagram.
“Surely dreams come true no matter how long it might take,happy to say that we did a collabo with one of Africa’s finest musicians @diamondplatnumz. It could not be more better than this,we produce good music for a living!!!!!Cant wait for August 12 #ALBUM LAUNCH #HICC.”
Diamond na Jah Prayzah wa Zimbabwe washoot video ya collabo yao Sauz
Reviewed by
on
12:48:00 AM
Rating: