Gabo afunguka juu ya tuhuma ya kutoka na Faiza Ally


Msanii wa filamu Gabo Zigamba, amefunguka kwa kusema kuwa hana mahusiano yoyote na msanii mwenzake wa kiwanda cha filamu Bongo, Faiza Ally. 

Muigizaji huyo ambaye hivi karibuni amefanikiwa kushinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume kwenye tamasha la Ziff 2016, amekiambia chanzo chetu kuwa hakuna mahusiano yoyote ya kimapenzi yatakayotokea kati yake na Faiza. 

“Faiza namjua kama producer wangu, amenishirikisha kwenye filamu yake ya Baby Mama Drama. Hakuna chochote wala hayatotokea mahusiano ya kimapenzi kati yetu,” amesema Gabo.
Gabo afunguka juu ya tuhuma ya kutoka na Faiza Ally Gabo afunguka juu ya tuhuma ya kutoka na Faiza Ally Reviewed by on 12:30:00 AM Rating: 5