Miaka mitatu imepita tangu alipofariki mwanamitindo, Reeva Steenkamp kwa kupigwa risasi na aliyekuwa mpenzi wake mwanariadha maarufu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius.
Baba mzazi wa mwanamitindo huyo amesimama mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kilipotokea kifo cha mwanae [Reeva Steenkamp] kutokana na afya yake kutokuwa nzuri. Ameiambia mahakama kuwa anaamini kabla ya kutokea kwa kifo cha binti yake wawili hao watakuwa waligombana na lazima Oscar Pistorius alipe kwa hilo lililotokea.
Mwanzoni mahakama ya mjini Pretoria ili muhukumu Oscar Pistorius kifungo cha gerezani cha mwaka mmoja kwa kosa la kuua bila kukusudia na baadaye kutumikia kifungo cha ndani ya nyumba yake kabla ya familia ya marehemu kukata rufaa ya kesi hiyo.
Kwa sasa kinachosubiriwa ni maamuzi ya hukumu kutoka kwa mahakama kutokana na kesi kubadilishwa kutoka kuua bila ya kukusudia mpaka kufikia kuwa kesi ya kuua kwa kukusudia.
Baba mkwe wa Oscar Pistorius asimama mahakamani kwa mara ya kwanza
Reviewed by
on
4:19:00 AM
Rating: