Siendi tena Afrika Kusini kushoot video – Adam Juma


Na sasa huenda ndoto ya wasanii wengine wenye nia ya kukwea pia na AJ ili kufanya video zao bondeni huenda zikawa zimefutika rasmi.  Ni kwasababu muongozaji huyo amesema kwa sasa (walau kwa sasa) hana mpango tena wa kwenda kufanya video zake nchini humo.
“Yaani sasa hivi mtu akiniambia anataka kwenda kushoot video South Africa siendi tena,” Adam alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka.
“Siwezi kwenda, sasa hivi nina commitment, watoto wanataka kwenda shule. Unalipwa hela ile ile kazi ambayo unaifanya hapa kwa siku moja, it doesn’t make any sense,” aliongeza.
“Mimi nimefanya video nyingi South Africa, lakini nimefanya kwasababu ya kuinvest, lakini sasa ukija kuangalia kwa faida kitu gani tunapata?”
AJ ameendelea kusisitiza kuwa uongozaji wa video kwa Tanzania bado haulipi na hiyo ni sababu iliyomfanya aache kufanya kazi nyingi kama zamani. Amesema kwa sasa atafanya kazi na wasanii ambao wako tayari kumlipa vile anavyotaka au mahitaji muhimu yanayohitajika kufanikisha wazo la video husika.
Hivi karibuni waongozaji wengine wa video nchini wameanzisha utaratibu wa kwenda na wasanii kufanya video Afrika Kusini. Mfano ni video ya Chafu Pozi ya Bill Nass na Pesa ya Madafu ya Jay Moe ambazo zote zilifanyika SA na kuongozwa na Msafiri wa Kwetu Studios.
Waongozaji wanadai kuwa sababu kubwa inayowapeleka Afrika Kusini kufanya video ni upatikanaji rahisi wa location ambapo kwa Tanzania huwawia vigumu kutokana na kutokuwepo utaratibu maalum na huku mamlaka zingine zikiwa na mchakato mrefu wa kuruhusu kutumiwa kwa maeneo husika.
Siendi tena Afrika Kusini kushoot video – Adam Juma Siendi tena Afrika Kusini kushoot video – Adam Juma Reviewed by on 10:44:00 PM Rating: 5