Frola Mvungi akiwa hospitali mapema mwaka huu
Baada ya H.Baba na mke
wake Flora Mvungi kuweka wazi mapema mwaka huu kwamba wanatarajia kupata mtoto
watatu, hivi karibuni Frola Mvungi ameonekana katika
picha hana ujauzito hali ambayo imewafanya mashabiki wake katika mitandao ya
kijamii kuhoji ilikuwaje.
Frebuari 8 mwaka huu, H.Baba ambaye ni baba wa watoto wawili, Tanzanite na Africa, alishare picha (hapo juu) katika mitandao ya kijamii zenye ujumbe kuhusu ugeni huo.
“Asante mungu kwa kila jambo #watoto nifaraja nakuombea muda ukifika ujifungue salama nakupenda mke wangu (1)tanzaniteone (2)Africa (???????) . Nitafutie jina la mwanangu Wa (3) nimuite nani?,” aliandika H.Baba.
Pia siku hiyo hiyo, mke wake Frola Mvungi alishere kwa mashabiki ujumbe mwingine kuhusu mimba hiyo.
“Hahahhahahahahhahaah nacheka kwa raha yaani nafuraha sana mana naona watu maneno yanawatoka kila kona..kwani kuzaa ni kosa?au kuna siku nimemuomba mtu hela ya kutunza wanangu??. Waja mna tabu sana,jamani hebu tusipangiane jinsi ya kuishi,,kingine siko nje ya ndoa na hata ingekuwa nje ya ndoa pia ni watoto wangu..mwakereka na nini??. Hhahaaaaaa yaani mtasema sana,” aliandika Frola Mvungi katika picha ambayo alipost instagram.
Baada ya mkanganyiko huyo, Bongo5 ilimtafuta H.Baba na kuzungumzia kauli hiyo ambayo iliwaacha mashabiki njia panda.
“Niliwauliza wananchi na mashabiki zetu kupitia insta wanichagulie jina la mtoto wa tatu 3 baada ya Africa na Tanzanite, watatu nimuite nani? . Tayari wao wamenipa majina yao kibao naendelea kuchagua jina moja. Mmesahau kabla ya mimba ya Tanzanite nilisema mwanangu ataitwa Tanzanite, kikubwa ndugu zangu endeleeni kunitafutia jina la mwanangu wa tatu kama ukitokea ujauzito,” alisema H.Baba.
Aliongeza, “Ni muda wakuwalea watoto wetu wawili wa kike na wakiume ashukuriwe Allah hii ni hatua kubwa sana kwangu kupata watoto wawili, nampenda sana mke wangu Flora Mvungi huyu ndiye malkia wangu wa nguvu kwangu mimi Tanzania nzima, hakuna kama malkia Florah Mvungi wengine malkia fake tuu. Bongo movie nzima ukitaja wadada wanao jiheshimu lazima jina la Mama Tanzanite linakuwemo kwa sababu anajiheshimu sana.
Frola Mvungi akiandaa kazi yake mpya
Frola Mvungi akiwa kwenye mahojiano hivi karibuni
Flora Mvungi alidanganya kuwa ana mimba au mimba iliyeyuka?
Reviewed by
on
4:26:00 AM
Rating: